Na Ayoub Julius - Lango la Habari
Aliyekuwa kocha wa timu ya Manchester united,Ajax,Barcelona na sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi kwa mara ya tatu Louis Van Gaal amefichua kuwa na Tezi dume.
Amesema kuwa amekuwa akitibiwa saratani hiyo kwa muda na hakutaka wachezaji wake walijue hilo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70 ameyasema hayo kwenye moja ya kipindi cha maonyesho ya televisheni kinachoitwa Humberto nchini Uhaolanzi siku ya Jumapili April 03, 2022 akiwa kwenye promosheni ya makala kuhusu maisha yake.
Louis Van Gaal ameshinda jumla ya mataji 20 katika maisha yake kama mkufunzi wa soka katika timu tofauti tofauti zikiwemo Ajax,Barcelona na Manchester United.