Breaking

Thursday, 21 April 2022

KMC FC YAZURU KABURI LA HAYATI MAGUFULI



Wachezaji, Viongozi pamoja na Benchi la ufundi la timu ya mpira wa Miguu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC  wamezuru katika kaburi la hayati Dokta John Joseph Pombe Magufuli nyumbani kwake Wilayani Chato Mkoani Geita ikiwa nisehemu ya kutambua na kuenzi mchango wake katika sekta ya michezo alioufanya enzi ya uhai wake.

Akielezea kuhusiana na Ziara hiyo, Afisa habari na mawasiliano wa KMC FC  Christina Mwagala amesema kuwa timu hiyo imetembelea Kaburi la Hayati Magufuli leo Alhamisi April 21, 2022 kwa kutambua mchango mkubwa ambao aliounesha kwenye sekta hiyo enzi ya uhai wake.


Amesema kuwa Timu hiyo pia imefika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya  ya chato pamoja na Mkurugenzi na kupata mapokezi mazuri pamoja na ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na kufanikisha kufika nyumbani kwa hayati Dk. Magufuli lakini pia kutumia uwanja wa Magufuli unaomilikiwa na Wilaya hiyo kufanya kwa ajii ya kufanya mazoezi.


“ KMC tunatambua mchango mkubwa ambao hayati Dk. Magufuli aliufanya enzi ya uhai wake katika sekta hii ya michezo, hivyo ndio mana tukaona wakati huu ambao Timu ipo huku kanda ya ziwa tufike nyumbani kwake kuzuru pamoja na kusalimia familia yake, lakini pia kufika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi ambapo kimsingi tumepata mapokezi makubwa na tunawashukuru kwa hilo" amesema Mwagala


Kwa upande wao wakazi wa Wilaya ya Chato wameonesha kufurahishwa na uwepo kwa timu hiyo kutokana na kujitokeza kwa wingi wakati wa mazoezi. 


"hii kwetu kama Timu tumechukua kama sehemu ya kutambua mchango wao kwetu na hivyo kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa pindi tutakapokuja huku kwa mara nyingine." Ameongeza Mwagala


KMC FC imeweka kambi Wilayani  Chato tangu Aprili 18 mwaka huu ikiwa ni mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar,uliopigwa Aprili 17 katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.


Aidha timu hiyo inaendelea kujiimarisha kuelekea katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania dhidi ya Geita utakaopigwa siku ya jumamosi ya Aprili 23 katika Uwanja wa Magogo saa 16:00 jioni.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages