Breaking

Sunday, 3 April 2022

KIPANYA AZINDUA GARI LINALOTUMIA NISHATI YA UMEME



Mchoraji katuni wa Tanzania, Masoud Kipanya amezindua rasmi gari lake ambalo ni la kwanza la umeme kutengenezwa hapa nchini.

Katika Uzinduzi huo uliofanyika jana April 02, 2022 katika Hoteli ya Dar es Salaam Serena na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara nchini. Kipanya amesema gari hilo ni 
aina ya KP A72eV na linatumia Nishati ya umeme.

amesema kuwa wazo lake binafsi la ubunifu ambalo lilimchukua miezi 11 kukamilika.

Gari hilo ambalo ni rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii nishati ya mafuta linaitwa Kaypee Motor na linachajiwa kwa saa sita kabla ya kutumika.

"Hili ni gari la nguvu sana ambalo ukinunua unapata na chaji yake," ameongeza Kipanya
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages