Breaking

Wednesday, 20 April 2022

KINANA AIPONGEZA WIZARA KWA KUHIFADHI UTAMADUNI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA




Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara. Mhe, Abdalahaman Kinana ame
pongeza juhudi zinazofanywa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuhifadhi utamaduni wa kiukombozi wa Bara la Afrika.


Kinana ametoa pongezi hizo leo Jumatano Aprili 20, 2022 baada ya kutembelea Ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jijini Dar es Salaam. 


Mhe. Kinana amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo uti wa mgongo wa taifa lolote na kusifu jitihada zinazofanywa na Wizara kwenye kuhakikisha utamaduni wa kiukombozi wa Bara la Afrika unaenziwa na kuhifadhiwa kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.



Kwa upande wake, Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa mpango wa Serikali kwa sasa ni kujenga makumbusho kubwa ya kisasa.



Aidha, amesema programu inaendelea na kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha mchakato wa kuyatangaza maeneo15 ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika yaliyopo nchini kuwa Urithi wa Taifa kwa kuyatangaza kwenye gazeti ya Serikali ili yalindwe kisheria.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages