Na Samir Salum-Lango la habari Blog
Kijana Thiame Bouna (19) kutoka Nchi ya Congo Brazzaville ameibuka Mshindi wa Kwanza na kuondoka na kitita cha shilingi milioni 20 katika Mashindano Makubwa zaidi ya kuhifadhi Qur'an Afrika 2022.
Mashindano hayo ambayo ni ya 22 yaliyo chini ya Al- hiqma Foundation kwa Usimamizi wa Sheikh Nurdeen Kishk yamefanyika leo Jumapili April 17, 2022 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa huku Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwakilishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Hussein Ally Mwinyi.
Katika mashindano hayo jumla ya washiriki 22 kutoka Nchi 22 za Afrika wameshiriki na kupatikana washindi saba ambapo kijana Thiame Bouna kutoka Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekuwa Mshindi wa Kwanza akipata alama 99.75 na kuondoka na Zawadi ya Shilingi Milioni 20.
Mshindi wa pili katika Mashindano hayo ni Abdullah Sengo Muhamad kutoka Nchini Uganda ambaye amepata alama 99.58 na kuondoka na zawadi ya Shilingi Milioni 12 wa tatu ni Yusuph Ishaq kutoka Nigeria aliyepata alama 99.33 na kushinda Shikingi Milioni 7.5.
Washindi wengine ni Irakiza Ismail kutoka Nchini Rwanda aliyeshika nafasi ya nne kwa alama 99.16 na kushinda Shilingi Milioni 5 na mshindi wa tano ni Ebd El Hamid kutoka Nchi ya Mauritania aliyepata alama 99.15 na kusinda shilingi Milioni 3.
Aidha, katika mashindano hayo ya makubwa zaidi ya Qur'an Afrika Imetolewa zawadi kwa Mshiriki mwenyw umri Mdogo katika mashindano hayo ambaye ni Umer Nuredin Kasim mwenye umri wa miaka 9 kutoka Nchini aliyepewa Dola 500 (1,161000Tsh) na pia imetolewa Zawadi kwa Msomaji wa sauti Nzuri ambaye ni Muhamed Ibrahim Ghonim kutoka Nchini MISRI naye amepewa 500USD.