Breaking

Tuesday, 26 April 2022

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA ILEMELA YAADHIMISHA MIAKA 58 YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI, KUCHANGIA DAMU



Na Samir Salum, Lango la Habari


Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilemela, timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na wananchi Mkoani Mwanza, imeadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya usafi wa mazingira na kuchangia damu katika Kituo cha Afya Buzuruga.

Hayo yamefanyika  leo Jumanne April 26, 2022 ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela katika maadhimisho hayo  Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilemela SSP Elisante Ulomi amesema kuwa kamati hiyo kwa kushirikiana na wananchi imeshiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira na kuchangia damu ili kuhamasisha na kuwasaidia wahitaji katika kituo hicho.

“katika kuadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kamati ya ulinzi na usalama inayoongozwa na mh DC Hassan Masalla tumekusanyika katika kituo chetu cha afya Buzuruga kwa ajili ya zoezi la usafi na kutoa damu lililoenda vizuri kwa kushirikiana na wananchi waliojitokeza kwa kiasi kikubwa”
amesema SSP Ulomi

Aidha, Kamanda Ulomi amewashukuru wananchi kwa kuonesha uzalendo baada ya kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo .

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga, Dkt William Mtinginya ameishukuru kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ilemela kwa kujitolea kufanya usafi na kuchangia damu huku akieleza kuwa zoezi la kuchangia damu limeleta matokeo chanya kwani kuna uhitaji mkubwa katika kituo hicho.

“tunaishukuru sana kamati ya ulinzi na usalama kwa kuchangia dam una hadi sasa tumepata uniti saba (7), tunaomba zoezi hili liwe endelevu na wananchi wazidi kujitokeza kwani bado tuna uhitaji mkubwa wa damu”
amesema Dkt Mtinginya

Naye Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Buzuruga Kusini Lenista Lwanga amewaasa wananchi kujiwekea utaratibu wa kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo yao na sio kusubiri hamasa kutoka kwa viongozi.

“Naomba suala la usafi liwe ni utaratibu na desturi kwetu, tusisubiri hamasa kutoka kwa viongozi au mpaka waje ndo tufanye usafi”
amesema

Watanzania leo wanaadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulioasisiwa April 26,1964 ambapo Maadhimisho hayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Uwajibikaji na Uongozi Bora, Tushiriki Sensa ya Watu na Anuani ya Makazi kwa Maendeleo Yetu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI-PICHA ZOTE NA SAMIR SALUM

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilemela SSP Elisante Ulomi  akifanya usafi katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Neema Kipeja katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza pamoja na wananchi wakifanya usafi katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga..


Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza pamoja na wananchi wakifanya usafi katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza pamoja na wananchi wakifanya usafi katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.

Baadhi ya wananchi wakichangia damu katika kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.

Baadhi ya wananchi wakichangia damu katika kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.
Baadhi ya wananchi wakichangia damu katika kituo cha Afya Buzuruga katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Kituo cha Afya Buzuruga.

PICHA ZOTE NA SAMIR SALUM-LANGO LA HABARI
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages