Breaking

Saturday, 9 April 2022

JESHI LA POLISI LATEKETEZA SHAMBA LA BANGI MTWARA



Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limebaini na kuteketeza shamba la Bangi lenye ukubwa wa Nusu hekari, katika mtaa wa Rwelu, kata ya Jangwani Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Akithibitisha tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo, amesema shamba hilo linamilikiwa na Abdulrahaman Bakari (42), ambaye alikutwa na Bangi Kilogramu 17 nyumbani kwake Mikindani ambaye alikamatwa March 27, 2022.

Kamanda Katembo amesema kuwa baada ya mtuhumiwa kushikiriwa alifanyiwa mahojiano na akakiri kuwa yeye na ndugu yake Himid Mohamed wanamiliki shamba la Bangi mtaa wa Rwelu.

Mnamo April 06, 2022 Mtuhumiwa aliongozana na maofisa wa jeshi la Polisi kwenda huko Rwelu kuonesha lilipo shamba hilo.

"alifika na kuonesha shamba linalofikia ukubwa wa nusu Hekari, katikati ya msitu wa asili likiwa limepandwa Bangi” Kamanda Katembo

Aomeongeza kuwa Jeshi la Polisi lilishirikiana na wananchi kuteketeza bangi hiyo.

Aidha amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea huku mtuhumiwa mwingine ambaye ni Himid Mohamed bado anatafutwa na Jeshi la Polisi.

"upelelezi utakapokamilika watuhumiwa wote watakaobainika kuhusika kutenda kosa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao.”


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages