Breaking

Saturday, 30 April 2022

EMEDO WAFANIKISHA UPATIKANAJI WA VIONGOZI WA TAWFA ILEMELA NA NYAMAGANA.

Wawakilishi wa TAWFA waliochaguliwa



Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo(EMEDO) limesimamia uchaguzi wa kuwapata Wawakilishi wa TAWFA wa wilaya za ILEMELA na NYAMAGANA Mkoani Mwanza.


Katika uchaguzi huo uliofanyika April 28, 2022 uliohudhuriwa na Vikundi 20 vya Wanawake Wavuvi na Wachakataji uliwachagua Angelina Deogratius na Catherine Fransis kuwa wawakilishi kutoka wilaya ya Nyamagana na Maimuna Rajabu na Ela Livingstone kuwa wawakilishi wa wilaya ya Ilemela.


Awali akizungumza na wanachama hao wa TAWFA Mgeni Rasimi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza Isack Ndasa aliwataka Wawakilishi watakaochaguliwa wahakikishe wanatafuta njia za kutatua changamoto za Wanawake Wavuvi na Wachakataji Ili go waone faida ya kazi hiyo.


Amesema kazi ya Uvuvi ni kazi yenye hadhi Kama kazi zingine na kuwataka Waache kuwa wanyonge mbele za wateja Kwa kuwa bila wao wateja hawawezi kupata mazao ya Samaki.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO  Editrudith Lukanga amewataka Wawakilishi hao waliochaguliwa kuhakikisha wanafanya kazi Kwa bidii na kuimarisha TAWFA  Ili iwe Taasisi yenye nguvu na inayotatua kero za Wanawake Wavuvi na Wachakataji.


Nae Mratibu wa Mradi huo Lucy Kilanga amesema jukumu la Wawakilishi hao wanne waliochaguliwa ni pamoja na kuwawakilisha wanakikundi 20 wa wilaya za Ilemela na Nyamagana katika ngazi ya mkoa ambapo watawakilisha changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi Kwa pamoja.


Shirika la EMEDO kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo Duniani pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wameanza kutekeleza mradi wa kuimarisha TAWFA kuangazia ngazi ya chini hadi ya juu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages