Na Tonny Alphonce - Mwanza
Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo Tanzania EMEDO kwa kushirikiana na Taasisi kutoka Wingereza inayohusika na masuala ya usalama kwenye maji na uokoaji RNLI wameingia mkataba wa miaka mitatu wa kusaidia jamii za wavuvi na majanga ya kuzama majini na kupoteza maisha.
Arthur Mugema Mratibu wa Mradi huo kutoka EMEDO amesema mradi huo utasaidia Jamii ya Wavuvi ambapo utafiti unaonyesha Kati ya Wavuvi laki Moja Jamii ya Wavuvi 231 wanapoteza maisha Kila Mwaka kutokana na kuzama ziwani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga amesema mradi utakao gharimu Zaidi ya Bilioni 2 utafanyika katika mikoa ya Mwanza,Kagera na Mara.
Naye Steve Wills Mkuu wa program RNLI amesema tatizo la Watu kufa maji ni kubwa Duniani hivyo Taasisi yao imeamua kufanya kazi na EMEDO Ili kutoa elimu kwa Jamii ya Wavuvi Ili waweze kujikinga na ajali za majini na kufanya Uvuvi salama.