Breaking

Sunday, 10 April 2022

DKT MABULA AKABIDHI VIFAA VYA UCHAGUZI CCM ILEMELA



Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amekabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili kutekeleza shughuli za chama cha mapinduzi CCM ikiwemo uchaguzi wa ndani unaoendelea katika baadhi ya kata zilizopo katika Jimbo la ilemela.


Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na karatasi, kalamu, mabati 22 yenye thamani ya laki nne na elfu themanini kwa kata ya Kahama, Luninga mbili na ving'amuzi vyake kwaajili ya vijiwe vya Kahawa vya Mwigulu kata ya Pasiansi na Kirumba vyenye thamani ya laki sita na elfu thelathini Viti hamsini vyenye thamani ya laki nane na elfu themanini.



Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo leo Jumapili April 10, 2022 Dkt Angeline Mabula amesisitiza kufanyika uchaguzi wa uhuru, haki na amani na kuongeza kuwa  ni wajibu wake kama Mbunge kuunga mkono juhudi hizo kwa kusaidia vifaa kwa kuwa si matawi yote au kata zote zenye uwezo wa kugharamia shughuli za uchaguzi 


"Kama Mbunge ni wajibu wangu kuwezesha matawi, kata au hata wilaya yangu vitendea kazi vya uchaguzi, Na hatutaishia hapa ule utatu wa Serikalini tutarudisha kwenye Chama tutajenga ofisi zetu za matawi na kata wanachama wajenge misingi, nitatoa tofali za ujenzi wa maboma na CCM wilaya kwa ushirikiano tutamalizia" Amesema


Aidha Dkt Mabula amemshukuru Rais Samia Kwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 29 kwaajili ya Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya hiyo Kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuingia kwake madarakani hivyo kuwaasa wanachama na wananchi Kwa ujumla kuzidi kuunga mkono Jitihada hizo. 



Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela, Nelson Meshack amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo huku akiwataka watendaji wa Chama kuvitumia vyema vifaa hivyo Kwa malengo yaliyokusudiwa.


Naye  Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Aziza
 Isimbula  amesema kuwa Kila Katibu ana wajibu wa kuwasilisha taarifa ya  shughuli za uchaguzi wa ngazi ya chini yake Kwa ngazi ya juu yake Kila siku zoezi linapokwisha hivyo kuja Kwa vifaa hivyo kutasaidia kuharakisha Utekelezaji wa zoezi hilo


Akihitimisha Katibu wa UVCCM kata ya Kahama Cosmas Lutebeka kwa niaba ya wanachama wa kata hiyo wameshukuru Kwa mabati yaliyotolewa na Mbunge huyo kwani yatasaidia kupunguza kero ya muda mrefu ya ukosefu wa Ofisi jambo lililochangia kurudisha nyuma shughuli za ujenzi wa Chama hasa kipindi Cha uchaguzi kinapofika.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages