Breaking

Monday, 18 April 2022

DKT MABULA AGAWA FUTARI NA ZAWADI ZA PASAKA KWA MAKUNDI MAALUM, AWAASA KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA



Na Samir Salum-Lango la habari 


Makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu,Wajane, Yatima na Wazee wametakiwa kujitokeza na kuhesabiwa siku ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo. 


Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula wakati wa zoezi la kugawa sakaka ya ftari na Zawadi za Sikukuu ya Pasaka Kwa makundi hayo ambapo amewasisitiza kuhakikisha wanajitokeza kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi Kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali kupanga mikakati ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo.


"Ndugu zangu nawaomba mpokee hiki kidogo nilichojaaliwa na Mungu kiwasogeze katika mwezi huu mtukufu wa mfungo na Pasaka Kwa wenzetu wakristo, Lakini pia niwaombe kama Mheshimiwa Rais Samia anavyosisitiza mjitokeze kushiriki zoezi la Sensa" Amesema Dkt Mabula


Dkt Mabula amewataka wananchi hao kuendelea kuwa wamoja na kuishi Kwa upendo kama Ilivyo Mila na desturi ya nchi sanjari na kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali.


Kwa upande wake Shekh wa wilaya ya Ilemela AbdulWarith Bin Juma amemshukuru mbunge huyo Kwa msaada alioutoa licha ya yeye kutokuwa muumini wa dini ya kiislamu lakini ameguswa kuwaunga mkono waislamu hivyo kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.


Moja ya wanufaika wa sadaka hiyo ambae pia ni  Yatima Rashid Balili mwanafunzi wa shule ya msingi Kayenze ndogo amempongeza Mbunge huyo na kumuomba kuendelea na moyo huo wa utoaji.


Dkt Mabula amegawa Ftar kwa Wazee, Yatima, Wajane huku Kila mmoja akipata Tambi, Kilo 4 za Mchele, Kilo 3 za Sukari, Kilo 2 za Ngano, Wajane waliongezewa Lita Moja ya mafuta ya kupikia huku Misikiti iliyopo Wilaya ya Ilemela ikipatiwa maboksi ya Tende.


Aidha ametembelea vituo vya watoto yatima na wasiojiweza ikiwemo kituo cha Fenelisco kilichopo kata ya Ilemela, kituo cha Hisani kata ya Buswelu pamoja na kituo cha Nitetee cha kata ya Kiseke ambapo amegawa zawadi za Pasaka ikiwemo Juisi, Mafuta, Sukari, Mchele na Ngano.


Jumla  ya vitu vilitolewa  vina thamani ya shilingi 38,500,000.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula amekuwa na utaratibu wa sadaka ya sadaka ya futari na zawadi  katika sikukuu za Pasaka na Krisimasi Kila mwaka ndani ya Jimbo lake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages