Breaking

Monday, 4 April 2022

BUNGE LIVE LARUDISHWA.. KUANZA KUONYESHWA KESHO APRIL 5



Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho Jumanne Aprili 5, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Jumatatu Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, amesema bunge live litaanza kesho katika mkutano wa saba wa bunge la bajeti.

Ameongeza kuwa vyombo vya habari ambavyo viko tayari kurusha matangazo hayo vitachukua kupita studio za bunge.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages