Breaking

Friday, 22 April 2022

BREAKING: RAIS MSTAAFU WA KENYA MWAI KIBAKI AFARIKI DUNIA




RAIS mstaafu wa Kenya, Mzee Mwai Kibaki aliyehudumu kati ya mwaka 2002 na 2013 amefariki dunia.


Taarifa ya kifo cha Mzee Kibaki imetangaza leo Aprili 22,2022 na Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba kwa taifa.


Mzee bKibaki alikuwa Rais wa Tatu tangu Kenya ipate Uhuru mwaka 1963.


Rais Kenyatta amemtaja kama kiongozi aliyekuwa katika mstari wa mbele kuimarisha uchumi wa Kenya.


“Mwai Kibaki atakumbukwa kwa weledi wake na bidii yake kazini. Kwa mujibu wa mamlaka yangu kama Rais wa Kenya, ninaamuru kwamba bendera ya Kenya itapeperushwa nusu mlingoti nchini na katika balozi zote za Kenya katika mataifa ya kigeni kuanzia leo Ijumaa hadi Rais mstaafu Kibaki atakapozikwa,” amesema Rais Kenyatta.


Kibaki aliingia Ikulu kupitia kwa tiketi ya National Rainbow Coalition (NARC) na akaapishwa Desemba 30, 2002, kutumikia taifa kama Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya.


Aidha,alihudumu kama kiongozi wa Taifa na Serikali hadi Aprili 9, 2013, alipokabidhi mamlaka kwa Rais Uhuru Kenyatta.


Rais Kenyatta amesema japo taifa linaomboleza, lakini pia ni muhimu kukumbuka wakati ambapo Kibaki alitumikia taifa pamoja na wakati mzuri aliofurahia na mkewe Mama Lucy Kibaki ambaye naye alitangulia mbele ya haki 26 Aprili 26, 2016 huko South Kensington, London, Uingereza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages