Breaking

Wednesday, 20 April 2022

AUAWA AKIGOMBANIA UNGA NA DAGAA





Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Bwembwela wilayani Muheza kwa tuhuma za kumuua, Eliasa Omari (55) kwa kumkata mapanga akidai kumuibia unga na dagaa.

Akithibitisha tukio hilo leo Jumatano Aprili 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Safia Jongo amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania unga na dagaa pamoja na simu iliyopelekea wawili hao kupigana kwa kutumia mapanga.

Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili Aprili 17, 2022 na kwamba mtuhumiwa yupo katika Hospitali ya Teule ya Muheza akipatiwa matibabu.

Kwa upande mwingine Kamanda Jongo amesema kuwa katika kuelekea katika msimu wa sikukuu ya Eid Jeshi la Polisi linaendelea operesheni za usalama barabarani ili wasafiri wanatumia barabara katika hali ya usalama
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages