Na Ayoub Julius - Lango la Habari
Mkufunzi wa Juventus na raia wa Italia Massimiliano Allegri amekili kuwa timu yake ya Juventus imejiondoa rasmi katika kinyanganyiro cha ubingwa wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Scudetto.
Yote hayo yamejiri baada ya mabingwa hao wa muda mrefu katika ligi ya Italia kupoteza mchezo wake hapo jana Jumapili April 03, 2022 dhidi ya Intermilan kwa bao 1-0 likifungwa na Hakan Calhanoglu kwa mkwaju wa penati katika dakika 5' za nyongeza kipindi cha kwanza.
Allegri amesema kuwa licha ya Intermilan kuwa nyuma kwa jumla ya alama 3 dhidi ya vinara wa ligi Ac Milan na Napoli anawapigia chapuo mabingwa watetezi hao kuwa washindi wa ligi hiyo ya Scudetto mwishoni mwa msimu huu.
Juventus wamecheza jumla ya michezo 31,wakishinda michezo 17,sare 8 na kupoteza michezo 6 na kufanikiwa kuvuna alama 59 wakiwa nyuma kwa jumla ya alama 17 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Ac Milan.
Vibibi kizee hao wa Turin wamefanikiwa kushinda taji hilo mara 36 katika historia ya ligi hiyo huku wakiweka rekodi ya kushinda taji hilo mara 9 mfulilizo kuanzia msimu wa mwaka 2011 mpaka 2019.