Breaking

Wednesday, 20 April 2022

AJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE ARUSHA




Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyo husisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema Mnamo April 19, 2022 muda wa saa nne usiku Gari aina ya  lori lenye namba za usajili T.250 CAA  lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini liligonga Gari 
ya Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY ikitokea Arusha mjini kwenda Karatu.


Kamanda Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa roli ambapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah.

Amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.




Ameongeza kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiri waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

Aidha, Kamanda Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages