Watu Nane wamefariki dunia na wengine 19 wamepata majeraha baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha magari mawili ambayo ni costear lenye namba za ushajili T287 CCY inayomilikiwa na kanisa Katoliki Njombe pamoja na Lori lililokuwa limebeba makaa ya mawe.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema ajali hiyo imetokea jana Jumapili April 24, 2022 majira ya jioni katika eneo la Igima Wilayani Wanging'ombe ambapo Coster hiyo ilikuwa imebeba Vijana wa Umoja wa Vijana wa Katoliki (UVIKANJO) jimbo la Njombe.
Kamanda Issa amesema waliofariki katika ajali hiyo ni Flora Mkinga, Teresia Mbuligwe, Benson Kigahe, Mariamu Mkulu, Eliezer Mwakipesile, Veronica Mwinuka, Alfred Mfuse na Frida Msigwa.
Aidha ameongeza kuwa majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa Njombe pamoja na hospital ya Mji wa Njombe Kubena.