
Na Samir Salum - Lango la Habari
Watu wanne wamefariki na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali ya basi la GEITA EXPRESS kugongana na Fuso mkoani Dodoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo imetokea jana Jumapili April 03, 2022 majira ya saa 10:30 Jioni katika kijiji cha Manchali Chamwino barabara ya Dodoma - Dar.
Ameeleza kuwa basi la Geita EXPRESS namba T 640 DLE linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Geita kugongana na Gari namba T 134 DXR aina ya Fuso.
Kamanda Lyanga ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni fuso kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari nakusababisha ajali hiyo.
Amesema majeruhi katika ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino na wanaendelea kupatiwa matibabu.
Amesema majeruhi katika ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino na wanaendelea kupatiwa matibabu.