Breaking

Sunday, 20 March 2022

WATUMISHI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI


Na Mwandishi Wetu 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji wote wa Wizara yake kujitafakari utendaji wao na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. 


Waziri Mchengerwa ameyasema haya wakati alipokuwa akifungua kikao cha kupitishwa kuhusu maandalizi ya Bajeti na Randama kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kamati ya bajeti leo Machi 20, 2022 katika ukumbi wa MAELEZO jijini Dodoma.


"Naomba niwatake watendaji wote kufanya kazi kwa kufuata maadili na taratibu za kazi za Serikali ili kuleta mafanikio  kwa wananchi kwa ujumla". Amefafanua Mhe. Mchengerwa



Amewataka Wakuu wa Idara wote kuwa na vikao vya kiutendaji na watumishi wao ili kuleta mageuzi  ya kiutendaji na kuwataka watendaji kufanya kazi kama timu  moja huku wakifungua milango ya wadau  kama wasanii ili  kujua  haki zao.

 

Watendaji tokeni waelezeni wasanii ili waweze  kujisajili ili waweze  kupata  haki zao na wapate  manufaa”. Amesisitiza Mhe. Mchengerwa


Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara imefanya mambo makubwa kwenye sekta za michezo, sanaa na Utamaduni na kwamba kinachotakiwa sasa ni kuendelea kufanya vizuri. 


Ametumia tukio hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kusaidia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali yake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages