Breaking

Friday 18 March 2022

BREAKING: WATUMISHI 52 WAFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUGHUSHI VYETI




Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza limeridhia kufukuzwa kazi kwa watumishi 52 ambao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga amesema leo Ijumaa Machi 18, 2022 kuwa watumishi hao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kitumishi ikiwemo kusema uongo na kughushi vyeti.

Makaga amezitaka idara za elimu ya msingi na Sekondari kujitathimini juu ya utendaji kazi huku akionya tabia ya wakuu wa idara hizo kuwahamisha wakuu wa shule na walimu wakuu wanaodaiwa kufanya ubadhirifu kwenye maeneo.

Makaga ametoa agizo kwa ofisa elimu Sekondari na msingi wa halmashauri hiyo kuwashusha vyeo walimu wakuu waliobainika kufanya ubadhirifu wa mali za umma katika vituo vyao vya kazi.

Diwani wa Kata ya Kasenyi, Triphone Marley amesema hakuna sababu ya watumishi wanaofanya makosa kwenye maeneo yao kuhamishwa vituo vya kazi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Binuru Shekidele amesema atasimamia nidhamu ya watumishi Ili kulinda hadhi yao kukemea maovu yanayofanywa na baadhi ya watu wa halmashauri hiyo.



Source : Mwananchi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages