Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Wafanyakazi wanawake wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO makao makuu tarehe 05/04/2022 wakiongozwa na Mhandisi Sofia Mgonja, wameadhimisha sikukuu ya wanawake duniani kwa kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya kufundishia katika chuo cha Ufundi Arusha ATC.
Akiongea katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Arusha ndugu John Mongela alisema amefurahishwa sana na TANESCO kuchukua jukumu la kukichagua Chuo cha ufundi Arusha kuja kutoa misaada ya vifaa vya kufundishia na kutoa hamasa kwa wanafunzi wakike wanaochukua masomo ya ufundi chuoni hapo.
"Tukio hili la leo ni somo kubwa sana, maana kuna sehemu unaweza kualikwa ukarudi kama ulivyokuja lakini Kwa hili mlilolifanya TANESCO la kuja kutoa misaada na kuleta shuhuda dhahiri za wahitimu waliomaliza hapa na Sasa ni wafanyakazi wanaohudumu ndani ya Shirika hili ni jambo linalotia matumaini " alisema Mongela.
Aliongeza kuwa ustawi unapopatikana kwa akina mama na watoto wa kike kwa ujumla huwa ni ustawi wa jamii nzima hasa ukizingatia wanawake wamekua mstari wa mbele katika kupigania maendeleo ya nchi.
"Bahati hii mliyoipata wanafunzi wa kike katika chuo hiki kupata ushuhuda wa mainjinia waliosomea chuo hiki ni bahati ya pekee sana, ikawe chachu ya kuwasukuma ili mfikie malengo yenu"alisema Mongela.
Naye Mhandisi Sofia Mgonja akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO alisema kuwa nia kubwa ya TANESCO kufika chuoni hapo ni kuwapa hamasa wanafunzi wa kike kumaliza masomo yao kwa kuwapa ushuhuda kutoka kwa viongozi wanawake wa TANESCO waliosoma katika chuo cha ufundi Arusha.
"Kwasababu wewe ni mwanamke usione kuwa haiwezekani, mmeona mifano halisi kuwa kuna wanawake wamesoma hapa na sasa ni viongozi" Alisema Mhandisi Mgonja.
Akitoa shukrani kwa niaba ya uongozi WA Chuo Mkuu wa chuo hicho Dk. Mussa Chacha ameeleza kuwa anaishukuru TANESCO kwa kukichagua chuo cha ufundi Arusha kuja kutoa hamasa na msaada wa vifaa mbalimbali vya kufundishia.
"Naishukuru TANESCO kwa kutuchagua kwani kuna taasisi nyingi lakini mmechagua kuja hapa, hii inaonyesha ushirikiano