Breaking

Tuesday, 1 March 2022

"WANAOTUMIA BODABODA KUPORA WASAKWE" - IGP SIRRO


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameagiza kufanyika kwa operesheni za kuwasaka na kuwakamata wahalifu wanaotumia pikipiki kupora pamoja na wahalifu wanaojihusisha na uvunjaji na kuiba mali za wananchi.

IGP Sirro amesema hayo leo Jumanne Machi Mosi, 2022 wakati alipofanya ukaguzi wa ghafla kwenye kituo cha polisi Stakishari, Tabata Shule na Kawe jijini Dar es salaam.

Katika Ziara hiyo IGP Sirro amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji kata na polisi kata kuendelea kuhamasisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuhakikisha matukio ya uhalifu yanapungua kwenye maeneo yao.

Aidha, amewataka madereva hasa wa pikipiki maarufu bodaboda kufuata masharti ya leseni zao na kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu wa kutumia nguvu.

Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages