Waandamanaji waliokusanyika nje ya ofisi ya serikali ya Uingereza kutaka Uingereza ilipe fidia kwa karne nyingi za utumwa, kabla ya ziara ya Prince William na Catherine, Duke na Duchess wa Cambridge, huko Kingston, Jamaica Machi 22, 2022 (Reuters) |
Mamia ya watu Nchini Jamaica wamekusanyika nje ya ubalozi wa Uingereza mjini Kingston, na kubeba mabango wakidai fidia kutokana na dhulma enzi za ukoloni wa waingereza.
Maandamano hayo yametokea jana Jumanne Machi 22, 2022 saa chache kabla ya Mwanamfalme wa Uingereza William na mkewe Kate kuwasili Jamaica kama sehemu ya ziara yao eneo la Carribean ikiwa ni sehemu ya ziara yake.
Ziara ya mwanamfalme huyo inaambatana na miaka 70 ya uongozi wa Malkia Elizabeth ambapo itakamilika kwa kuizuru Bahamas.
Mwanaharakati aliyeandaa maandamano hayo Dokta Rosalea Hamilton, amesema kuna makosa ya kihistoria yaliyofanyika na yanapaswa kushughulikiwa huku akidai kuwa Uingereza wanatakiwa kuomba msamaha na kuwalipa fidia.
"Ninataka Uingereza watambue kwamba wamefanya uhalifu mkubwa dhidi ya watu wa Afrika na lazima waombe msamaha na kurudisha kile walichochukua kutoka kwa mababu." Amesema
Barua iliyochapishwa kabla ya ziara hiyo, na kutiwa saini na wanasiasa 100 wa Jamaika, wanasheria na wasanii, ilisema fidia ni muhimu "kuanza mchakato wa uponyaji, msamaha, upatanisho na fidia."
Serikali mwaka jana ilitangaza mipango ya kuiomba Uingereza fidia kwa kuwasafirisha kwa nguvu Waafrika wanaokadiriwa kufikia 600,000 kufanya kazi katika mashamba ya miwa na migomba ambayo yalitengeneza bahati kwa watumwa wa Uingereza.
Mbunge wa Jamaica Mike Henry amependekeza fidia ya pauni bilioni 7.6. Akieleza kuwa idadi hiyo imetokana na malipo ya pauni milioni 20 ambayo serikali ya Uingereza ilifanya mwaka 1837 kuwalipa fidia wamiliki wa watumwa katika makoloni ya Uingereza kwa ajili ya kuwakomboa watu waliokuwa watumwa kufuatia kukomeshwa kwa utumwa mwaka 1833.

Mamia kwa maelfu ya Waafrika waliokuwa watumwa walifanya kazi ngumu nchini Jamaika zaidi ya miaka 300 ya utawala wa Waingereza.
Jamaica inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru mnamo mwezi Agosti.