Wachawi wa Ukraine wanakusudia kufanya matambiko matatu yatakayomuondoa madarakani Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Kwa mjibu wa shirika la habari la UNIAN likiinukuu taarifa ya duka la Witch Cauldron lililopo mjini Kiev.
"Mnamo Machi 31, siku ya 29 ya mwezi, siku ya rushwa na laana, sisi, wachawi wa Ukraine kwa kushirikiana na washirika wa kigeni, tutafanya ibada ya kumwadhibu adui wetu - Vladimir Putin," wachawi hao walichapisha kwenye akaunti yao ya Instagram.
Wachawi hao wamesema tambiko hilo litafanywa kwa awamu tatu; ya kwanza itafanyika Ukraine katika Mlima wa Bald nje ya Kiev, hadi sasa, baadhi ya wachawi 13 wameonyesha nia ya kushiriki katika mpango huo.
Tambiko la pili litafanyika "Avic" Ibada hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kwa kuunda "gunia la jiwe" kwa rais wa Urusi, ambaye atakabiliwa na kutengwa, kuondolewa madarakani na kupoteza uungwaji mkono ndani ya watu anao waongoza.
Ingawa wachawi hawakutaja ni lini hasa tambiko hilo litaanza, shirika la utangazaji la Urusi lilisema katika taarifa yake mapema Ijumaa kuwa mipango ya wachawi tayari imeingia dosari.
Katika taarifa iliyofuata ya Instagram, wachawi hao walikiri kwamba "adui" wao ana "ulinzi mkali" na ibada hiyo inaweza kuwadhuru wale watakaoshiriki. Wachawi hao wamerudia azimio lao la kuifanya, wakisisitiza kwamba "wanajua wanachofanya."