Breaking

Wednesday, 2 March 2022

WANAJESHI 5800 WA URUSI WAUAWA , VITUO 1235 VYA MAJESHI YA UKRAINE VYATEKETEZWA




Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa katika siku ya sita ya opereseheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imeangamiza vituo zaidi ya 1,300 vya kijeshi vya Ukraine na aina kwa aina ya miundombinu ya kijeshi ya nchi hiyo.


Wizara ya Ulinzi wa Russia jana Jumanne iliwaambia wandishi wa habari kwamba katika opresheni maalumu ya kijeshi ya Russia yenye lengo la kuipokonya silaha Ukraine, Moscow imefanikiwa kuangamiza vituo 1325 vya kijeshi vya Ukraine vikiwemo vituo 43 vikuu na vituo vya upashaji habari za kijeshi.


Hayo yameripotiwa katika hali ambayo, wajumbe wa Russia na Ukraine wanatarajiwa kukutana tena jioni hii katika mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi mgogoro wa hivi sasa baada ya awamu ya kwanza ya mazungumzo hayo kumalizika juzi Jumatatu bila ya natija yoyote.

Aidha vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimesema takwimu za awali zinaonesha vikosi vya kijeshi vya Urusi vimepata hasara kubwa tangu mwanzo wa uvamizi huo.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza inaamini kwamba vikosi vya Moscow vimepata hasara kubwa wakati wa uvamizi wake nchini Ukraine.

Jumla ya hasara ya Urusi inayodaiwa na Ukraine kufikia sasa ni pamoja na: Wanajeshi 5,840, Ndege 30, Helikopta 31, Mizinga 211 na Magari 862 ya kivita (APVs)

-Pia Tangi 60 za mafuta , Magari 355 na Roketi 40 za MLRS zilizokamatwa

Mykhaïlo Podoliak, mmoja wa wapatanishi wa Ukraine amesema, pande mbili katika mazungumzo hayo zimeanzisha mfululizo wa vipaumbele na maudhui ambazo zinahitaji baadhi ya maamuzi ya ngazi za juu kabla ya kuingia kwenye awamu ya pili ya mazungumzo hayo.




Tarehe 24 mwezi ulioisha wa Februari, Rais Vladimir Putin wa Russia alitoa amri ya kushambuliwa kijeshi Ukraine na kusisitiza kuwa, Moscow haina nia ya kukalia kwa mabavu ardhi ya nchi yoyote ile.

Operesheni hiyo ilianza siku chache baada ya Russia kutangaza kutambua rasmi uhuru wa majimbo mawili ya Donestk na Luhansk ya mashariki mwa Ukraine.

Russia inasema Ukraine imevunja makubaliano ya Minsk ya mwaka 2014 na 2015 kati ya Kyiv na majimbo yanayopigania uhuru wao na kwamba Ukraine ndiyo iliyoanza kutumia nguvu za kijeshi kushambulia majimbo yaliyojitangazia uhuru.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages