Breaking

Tuesday, 22 March 2022

SERIKALI KUFUATILIA UWEPO WA AINA MPYA YA KIRUSI CHA UVIKO-19






Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali inafuatilia uwepo wa aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19 kilichothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Waziri Ummy aliyasema hayo jana Jumatatu Machi 22, 2022 jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya wataalamu wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na ugonjwa mahututi yanayofanyika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Fahamu Muhimbili (MOI).

Amesema kirusi hicho kinajumuisha kirusi cha Delta na Omicron, ambacho kimejiunda na kuwa kirusi kipya cha Omicron BA.1.


Amesema wizara yake inaendelea kufanya utafiti kuwapo kwa kirusi hicho na kwamba ameshawaelekeza wataalam kufatilia suala hilo.


"Serikali imeshachukua hatua za kuendelea kuchunguza na kujua kwamba kimeingia Tanzania au bado lakini nchi nyingine tayari wameshathibitisha." Amesema Waziri Ummy.

Waziri ummy ameendelea kuwasihi watanzania kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa kuwa bado Corona ipo Tanzania.

Aidha amewata watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kama wanavyoelekeza wataalamu ikiwepo kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa barakoa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages