Breaking

Monday, 21 March 2022

SERENGETI GIRLS YAIBAMIZA BOTSWANA 4 - 0, WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA




Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza Timu ya Taifa U-17 Serengeti Girls kwa  kuishinda timu ya Taifa ya Botswana mabao 4-0 katika  mchezo wa kufuzu kucheza kombe la Dunia 2022 nchini India. 


Mhe. Mchengerwa amesema  timu ya Serengeti Girls inasitahili pongezi kwa kuwa imeendelea kuiheshimisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.


"Nilipoitembelea kambini wiki iliyopita  huko Zanzibar nilifanya vitu viwili; niliwapa jina rasmi la Serengeti Girls na niliwapa mikakati, ninafurahi kuona wamelitendea haki jina hilo na mikakati tuliyowapa wameitekeleza". Ameeleza Waziri Mchengerwa.




Timu ya Taifa ya Wanawake U17 ya Serengeti Girls imeweza kufuzu mzunguko unaofuata baada ya kuwatoa Botswana kwa jumla ya magoli 11 kwa 0 baada mechi ya awali iliyopigwa Zanzibar kushinda 7-0 na  jana marudiano kushinda magoli 4-0 yaliyofungwa na Neema Paul 1 na Clara Luvanga 3.


Baada ya mchezo huu mchezo unaofuata Serengeti Girls watapambana na Timu ya Taifa ya Burundi.




Mashindano ya dunia ya Soka ya Wanawake chini ya miaka 17 yanafanyika Oktoba 2022 India baada ya kupata wawakilishi wa FIFA toka kila bara.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages