Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kabla ya kufungua rasmi Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach, katika hafla iliyofanyika eneo la Agha Khan Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa pamoja na Balozi wa Korea hapa nchini Kim Sun Pyo kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila pamoja na viongozi wengine wa Serikali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakitembelea na kukagua Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo tarehe 24 Machi 2022.
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa daraja jipya la Selander (Tanzanite) ni muendelezo wa jitihada za Serikali kuimarisha miundombinu ili kukabiliana na kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Rais Samia amesema hayo Ieo Alhamisi Machi 24, 2022 wakati wa hafla ya ufunguzi wa daraja hilo la Tanzanite lenye urefu wa kilomita 1.03 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema, dhamira ya Serikali ni kuifanya Dar es Salaam kuwa Jiji la kisasa na la kipekee, kusaidia kupunguza foleni pamoja na kuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za uchumi na biasharaJijini humo.
Ameeleza kuwa ujenzi wa barabara na madaraja unagharimu fedha nyingi, hivyo amewasihi wananchi kutunza miundombinu.
Aidha Rais Samia amemwagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kubadilisha alama ya mwenge iliyowekwa kwenye daraja mpya la Tanzanite na kuweka alama ya madini hayo itakayoendana na jina la daraja hilo.
“Niseme kidogo Waziri ushauri nilioupata kutoka kwa wananchi daraja hili tunaliita la Tanzanite lakini alama tuliyoiweka ni alama ya mwenge. Pamoja na kutambua mwenge ni tunu yetu adhimu wananchi wangependa sana kuona alama ya tanzanite pale ilipo alama ya mwenge ili liendane na jina la daraja hili,” amesema Rais Samia
Gharama za ujenzi wa Daraja hilo la Tanzanite ni Dola za Kimarekani Milioni 123.032 ambazo ni fedha za mkopo nafuu kutoka Serikali ya ya Korea kupitia Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF) na Dola za Kimarekani Milioni 4.233 ikiwa ni mchango kutoka Serikali ya Tanzania.