Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kutunza mazıngira,
hususani uoto wa asili kwa kuepuka kukata au kuchoma miti ovyo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia Rais ametoa wito huo leo wakati akihutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji kilichofanyika
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema katika maeneo ya vijijini, chemichemi nyingi za maji pamoja na baadhi ya mito imetoweka kutokana na
uharibifu wa mazıngira, na pia kutokana na kufanya shughuli nyingine za
kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya maji kufanya utafiti na kuangalia uwezekano wa kutumia maji ya Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya baadae katika jiji la Dar es Salaam.
Awali akizindua mradi wa maji uliogharimu
shilingi Bilioni 18 utakaosambaza maji kutoka Mboga, Chalinze hadi Mlandizi
Wilayani Bagamoyo, Rais Samia ameikopesha Wizara ya Maji shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi ili yaweze kuwafikia kwa
haraka.
Amewataka wananchi kuhakikisha wanalipa ankara za huduma ya maji wanayopatiwa ili Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Dar es Salaam (DAWASA) iendelee kutoa
huduma kwao.