Na Samir Salum - Lango la habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali ya basi iliyoua Watu 22 huku 32 wakijeruhiwa ajari iliotokea eneo la melela kibaoni barabara ya iringa-morogoro baada ya basi la kampuni ya Ahmed likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana na Lori la lilikokuwa likisafiri kwenda nje ya nchi.
Soma Zaidi AJALI YA BASI YAUA 22 NA KUJERUHI 38 MOROGORO
Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Machi 18, 2022 majira ya saa 11 jioni, eneo la Melea Jibaoni, njia panda ya Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro - Iringa na kusababisha vifo vya wanaume 15 wanawake 6 na mtoto mmoja wa kiume.
Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuongeza juhudi ya kuthibiti ajali na kuwaasa madereva kuzingatia sheria.
Aidha ametoa salamu za pole kwa wafiwa na anaugana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.