Na Samir Salum
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na vingozÄ° wa dini mbalimbali kwa ajili ya kujadili masuala ya maendeleo ya nchi.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus ameeleza kuwa kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Machi 02, 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Miongozi mwa masuala Waliozungumza na Rais Samia Viongozi hao wa dini wamependekeza kuwepo na mjadala mpana kuhusu mfumo mpya wa elimu utakaokidhi mahitaji ya sasa kwa maana ya kutozalisha jamii ya wahitimu walioandaliwa kuajiliwa peke yake.
Wameomba kutotozwa kodi
ya mapato kwenye fedha ambazo zinapatikana kama misaada ya hiari ya wanachama
na wafadhili kwa ajili ya kuendesha huduma zisizo za kibiashara zikiwemo
huduma za wajane na yatima.
Aidha wametoa wito kwa serikali kuhamasisha upandaji miti ya asili badala ya miti na mbegu kutoka nje ambazo nazo zinahatarisha usalama wa afya za wananchi ikiwa ni sehemu ya kupewa kipaumbele Suala la uchafuzi wa mazingira.
Pia, wametumia mkutano wao na Samia kuomba mamlaka husika kutumia busara ili kuangalia namna ya kumaliza kesi Inayomkabili kingozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake.
Ujenzi wa mahusiano bora kwa nchi
jirani na jamii ya kimataifa, fursa za uongozÄ° kwa wanawake na kuulinda
Muungano ni baadhi ya mambo aliyopongezwa Rais Samia na vingozÄ° hao wa
dini.