Breaking

Wednesday, 30 March 2022

RAIS SAMIA AREJESHA TOZO YA SHILINGI 100 KWENYE MAFUTA



Rais Samia Suluhu ameagiza tozo ya TZS 100 iliyokuwa imetolewa kwenye mafuta irejeshwe kwa sababu hesabu zake tayari zilikuwa zimepigiwa kwenye bajeti.


Rais samia ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 30, 2022 wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU.


Amesema suala la upandaji wa bei za mafuta yamekuwa yakipanda tangu katikati ya mwaka jana na kwamba walichukua hatua yakupunguza tozo kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi.


Amesema kwa mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta duniani, kuondoa TZS 100 hakutasaidia, ila kutainyima serikali mapato.


“Kipindi hiki cha pili mafuta yamepanda kwa Sh. 156 kwa lita Waziri akaona nikitoa Sh. 100 yapande kwa Sh. 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi kwamba ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge” amesema Rais Samia


“Tumekaa kama serikali tumerekebisha ile Sh. 100 iliyotoka nimeagizwa irudishwe, Tathimini tuliyoifanya hata kama ile shilingi tukiitoa kwa mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta duniani bado isingekuwa na impact ila tungejikosesha kile ambacho tunakusanya” amesisitiza Rais Samia


Aidha Rai Samia amewataka wabunge, mawaziri wanaosimamia sekta hiyo kuwaambia ukweli wananchi kuwa vita ya Russia na Ukraine imepandisha bei ya mafuta.


Wizara ya Nishati iliondoa tozo hilo Februari 28, 2022 ikisema uamuzi huo umetokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na vita kati ya Russian na Ukraine.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages