Breaking

Friday 18 March 2022

RAIS MWINYI ATUNUKIWA TUZO YA KISWAHILI NA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO



Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo  Machi 18, 2022 imemtunukia tuzo ya heshima ya Kiswahili, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Zanzibar wakati alipokuwa  akifunga Kongamano la Pili la Idhaa ya Kiswahili jijini Arusha.


Tuzo hiyo ya heshima ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili iliyokabidhiwa na  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Serikali.




Rais Mwinyi ameishukuru Serikali kwa kumtunukia tuzo hiyo na kueleza kuwa atampatia ari zaidi ya kuendelea kukitangaza Kiswahili duniani.


Aidha, ametoa wito kwa Kamati ya Maandalizi kufikiria kufanyia Kongamano la tatu mwakani Zanzibar  ili kuleta maana zaidi ya kueneza na kuendeleza Kiswahili.


Kongamano hilo lilihudhuriwa na takribani washiriki 200 kutoka idhaa mbalimbali za Kiswahili duniani.


Akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameiomba Serikali kuweka  vituo vya Utamaduni kwenye Balozi za Tanzania nje ya nchi ili kukuza na kuendeleza Kiswahili.


Katika  Kongamano hili Mhe. Rais Mwinyi alipata fursa ya kuzindua mfumo wa kufundisha Kiswahili pamoja na kutoa vyeti vya kuwatambua washiriki na wadhamini.


Kongamano hili limerushwa mbashara na TBC, ZBC na vituo kadhaa vya Redio na televisheni.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages