Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametenguwa uteuzi wa viongozi watatu.
Waliotenguliwa ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Mji Mkongwe, Madina Haji Khamis.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi Zena Said utenguzi wa viongozi hao umeanza leo Alhamisi Machi 3, 2022.
Mwingine aliyepitiwa na panga hilo ni Mkurugenzi Mkuu Afya, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Dk Abdulla Suleiman Ali.
Mwingine ni Mkurugenzi Mkuu wa Sekretarieti ya Tume ya Ushindani Halali wa Biashara, Mohammed Jaffar Jumanne.