Na Samir Salum
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Yusuf Juma Mwenda kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kuanzia leo Machi Mosi, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa ikiyitolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu mkuu kiongozi Mhandisi Zena Saidi kwa vyombo vya habari amesema kuwa uteuzi huo umeanza leo Jumanne Machi Mosi 2022.
Ameeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Yusuf Juma Mwenda alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kutengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.