Watu saba wakiwemo watano wa familia moja Mkoani Katavi wamefariki baada ya kupigwa na radi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 4, 2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame ameelezea kuwa tukio la watu watano wa familia moja limetoka Machi 2, 2022 majira ya usiku wakiwa wamelala.
Amesema kuwa wakazi hao ni wa wa Kijiji cha Kamsisi Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
“Waliopoteza maisha ni Masalu Sengule (32) Muri Shija (25) Nkiya Masalu (7) Vumi Masalu (5) na Mariam Masalu umri wa miezi mitano” amesema ACP Makame
Aidha, Kamanda Makame amesema kuwa watu wengine wawili wakazi wa Mlibanzi wilayani Tanganyika mkoani humo wamefariki kwa kupigwa na radi wakiwa shambani.
Amewataja marehemu hao kuwa ni Elizabeth Nywandwi (13) na Faineth Mihani (37)”.