Breaking

Saturday, 19 March 2022

RADI YAUA NG'OMBE 28 KATAVI



Ng'ombe 28 za wafugaji watano wamekufa kwa kupigwa radi katika Kijiji cha Kabage wilayani Tanganyika.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Maico Kushoka amesema tukio hilo limetokea Alhamisi Machi 17, 2022 majira ya 12 jioni walipokuwa wakitoka malishoni, ambapo wachungaji hao walikuwa na ng’ombe 42 kati yao 28 walipigwa radi.

"Mvua ilikuwa inanyesha ikiambatana na radi, waliona mwanga wa radi wakatawanyika baadaye walimuona ng'ombe mmoja amekufa, wakaenda kutoa taarifa nyumbani.

"Baada ya kurudi waliona wengine 27 wamekufa, ng'ombe 9 walikuwa mali ya sita Busheneli, Mwanamazuri ng'ombe 8, Masanja 5, Makune 4 na wawili hakutambulika mmliki" amesema.

Kushoka amesema kiongozi wa kimila amefika eneo hilo kufanya tambiko la kimila ambapo wananchi walichinja na kugawana kitoweo.

"Tukio hili ni la pili kutokea mwaka 2018 walikufa ng'ombe wanne kwakupigwa radi, tukio la juzi nyumba tatu zimebomoka na barabara imekatika lakini hakuna madhara kwa binadamu," amesema.




Source: Mwananchi

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages