Watu wawili ambao ni Mama na Mtoto wamefariki baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha Mkoani kigoma.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amewataja marehemu hao kuwa ni Betha Zabron (44) na mwanae Lovenes Kulwa (01) Wakazi wa Kijiji cha Matyazo, Wilaya na Mkoani Kigoma.
Kamanda Manyama amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumatatu Machi 21, 2022 majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa ikinyesha ambapo Mama na Mtoto wake walikuwa shambani huku Baba wa Familia, Kulwa Abela alipata mshituko na kujeruhiwa.
Aidha, Watu wawili ambao ni Zubery Selemani na Yaulimwengu Kametelu wakazi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, wamejeruhiwa pia kwa radi na wanaendelea kupatiwa matibabu.
Aidha, Watu wawili ambao ni Zubery Selemani na Yaulimwengu Kametelu wakazi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, wamejeruhiwa pia kwa radi na wanaendelea kupatiwa matibabu.