Breaking

Monday, 28 March 2022

PROF. NGOWI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI




Mwanazuoni mbobezi wa masuala ya uchumi na mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi amefariki dunia leo Jumatatu Machi 28, 2022 baada ya gari lao kuangikiwa na kontena eneo la Mlandizi akiwa njiani kuelekea Morogoro.


Katika ajali hiyo, Prof Ngowi alikuwa na dereva wake ambaye naye amefariki dunia.
Dereva 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza imetoka eneo la Mlandizi mkoani Pwani ikihusisha magari matatu.


"Ni kweli ajali imetokea leo saa 12 alfajiri ikihusisha magari matatu aina ya Noah, Land Cruiser alilokuwa anasafiria yeye na lori ambalo ndio chanzo cha ajali lilihama njia na kuiangukia Noah ubavuni kisha kuilalia gari ya Ngowi," amesema.








Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages