Breaking

Thursday, 3 March 2022

NAIBU WAZIRI MARYPRISCA AONYA WATENDAJI RUWASA SIMIYU KUCHAFUANA KWA AJILI YA MADARAKA

 


Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Maji Vijini, (RUWASA) Mkoani Simiyu, akiwataka kuacha mara moja tabia ya kuchafuana kwa lengo la kusaka madaraka.


Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkula wilayani Busega wakati akikagua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili unaotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuhdumia wananchi wa vijiji vitano vya eneo hilo.


Amewataka watendaji hao kuanza kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta tija na kudai kuwa tabia ya kuchafuana itasababisha halmashauri hiyo kuwapoteza viongozi wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kupata maji safi na salama.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages