Na Mwandishi Wetu
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Jumapili Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema kuwa wanafamilia hao hawakuelewana wakati wa mazungumzo yao ambapo ilitokea sintofahamu ikapelekea ugomvi kutokea ndipo Mande Emanuel (30) aliamua kumkata na panga mumewe Dotto Enos (35) na kumjeruhi vibaya.
“Alipogundua mume wake anaweza kufa akahofia kupata kesi ya mauaji, alizunguka nyuma ya nyumba yao akapasua kitenge chake akajinyonga, mume alipelekewa hosptali ya rufaa mkoa kutibiwa,” amesema Kamanda Makame
Kamanda makame amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo.