Mchungaji wa kanisa la Pentekoste eneo la Mlimani City Lwanzari kata Ng'ambo manispaa ya Tabora amezua taharuki baada ya kuwachangisha fedha wananchi wa maeneo hayo kwa ahadi kwamba anawajengea kituo cha kulea watoto (Compasion).
Imeelezwa kuwa wazazi walichangishwa shilingi elfu 4,000 kwa mtoto mmoja kwa ahadi kwamba kuna wafadhili wazungu watakuja kuwaondoa wazazi kwenye umasikini na kuwasaidia kusomesha watoto.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Ng'ambo Adam Ntirihungwa amedai kuwa mchungaji huyo alianza uchangishaji fedha kwa muda mrefu hadi mnamo Machi 16, 2022 ambapo viongozi wa serikali ya mtaa walimhofia.
Amesema kuwa mchungaji huyo mwanzilishi wa wazo hilo alipobanwa na viongozi hao alikubali kurejesha fedha za wananchi lakini leo Ijumaa Machi 18, 2022 amekimbilia kusikojulikana baada ya kuachiwa kwa dhamana huku watu wengine wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Lango la habari imezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi