Breaking

Friday 18 March 2022

MBOWE ATOA TAMKO JUU YA WABUNGE 19 WA VITI MAALUM



Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Chama hicho kupitia kamati kuu akijawahi kuteua wabunge 19 wa viti maalum. 

Mbowe amesema hayo leo Ijumaa Machi 18, 2022 jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Machi 16.


Amesema Baraza Kuu litakaa mwezi ujao tarehe 25 na kama kuna rufaa zao tutaziona.


“Chadema haijawahi kuteua Kamati Kuu na ninarudia tena leo Chadema haijawahi kuteua wabunge wa viti maalumu” amesema Mbowe

Amesema kuwa Spika wa Bunge ameshaandikiwa barua na anajua wabunge 19 wa viti maalumu sio wabunge walioteuliwa na chama hicho.

Aidha  Mbowe ametaja mambo matatu waliyozungumza na Rais Samia Suluhu Hassan walipokutana Machi 04, 2022 baada ya kutoka gerezani, ikiwamo kujadili njia bora ya kutafuta amani na suluhisho katika kufanya siasa.

"Nilipokwenda kukutana na Rais Ikulu, tulichokizungumza ni kitu kimoja tu cha msingi, kwamba tulikubaliana kutafuta njia za haki, za mazungumzo, za mashauriano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa letu" 

Amesema; “Tulikubaliana aache kuzungumzia neno amani azungumze neno haki. Jambo la tatu nilimfahamisha yeye apende au mtu mwingine Chadema ni Chama Kikuu cha Upinzani huwezi kukiacha nje.”

Akisisitiza kuhusu hoja hiyo, amesema chama hicho kipo kila mahali na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vingine haviwezi kuinyamazisha.

“Mambo mengine Nilimwambia tutazungumza baada ya kukutana na chama changu,” amesema.



Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages