Breaking

Saturday 19 March 2022

MARUFUKU UVUTAJI WA SIGARA HADHARANI - TMDA






Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Kanda ya Kati, Sonia Mkumbwa amesema watumiaji wa bidhaa za Tumbaku watatakiwa kutengewa maeneo maalum ili kulinda Afya za watu wengine wasiotumia.

Amesema ni marufuku matumizi ya sigara na bidhaa za Tumbaku katika maeneo yasiyo rasmi na maeneo ya hadhara.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku kifungu cha 12(2), maeneo yasiyoruhusiwa ni pamoja na maktaba, sehemu za ibada, kambi, katika shughuli za michezo na burudani na sehemu zinazouza vyakula, ofisi, vyombo vya usafiri, mabanda ya maonesho, masoko, maduka na sehemu nyingine maalum kwa ajili ya kukutania watu.

Aidha, kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu yeyote anayemiliki maeneo yaliyokatazwa anapaswa kutenga sehemu kwa ajili ya wavutaji.

"Chumba kitakachokuwa kimetengwa kwa ajili ya uvutaji Sigara kitatakiwa kuwa na mfumo wa kutolea moshi nje na kuweka maandishi ya 'No Smoking' na 'Hairuhusiwi kuvuta Sigara katika maeneo pasipoŕuhusiwa," inasema sheŕia hiyo.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages