Breaking

Wednesday, 30 March 2022

MAMA AUA MWANAE KWA KUMNYONGA NA KUMJERUHI MWINGINE - MANYARA




Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Mwanamke mmoja aitwae Paschalina Geay (59)  kwa tuhuma za kumuua Mtoto wake wa kiume umri wa miaka 6 kwa kumnyonga shingo na Kisha kumjeruhi katika paji la uso kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara ACP Limited Mhongole amesema tukio hilo limetokea Machi 26, 2022 ambapo mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkazi wa mtaa wa Angoni "A" wilaya ya Babati  alitekeleza mauaji hayo kwa kumnyonga Nada Peter (06) na kumeruhi kwwnye paji la uso.

Kamanda Mhongole ameeleza kuwa baadae mtuhumiwa alimshambulia Mtoto wake mwingine Dawii Peter (4) kwa kumpiga maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mkono wa kulia na lengo ikiwa ni kumuua pia Mtoto huyo.


 Aidha, amesema uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa huyo ana matatizo ya afya ya akili na hivyo upelekezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages