Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amependekezwa na Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa akishik nafasi hiyo Philip Mangula kuwasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia ngazi.