Breaking

Thursday, 31 March 2022

KATIBA YA SASA HAINA TATIZO , WANAOITAFSIRI HUTOA MAANA TOFAUTI - NAIBU WAZIRI PINDA






Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Godfrey Pinda amesema Watanzania waipe muda Katiba iliyopo ili iangaliwe maeneo yanayokera ili kuimarishwa, kwa sababu haina tatizo lolote isipokuwa wanaoitafsiri hutoa maana tofauti.

Pinda alitoa msimamo huo Machi 29, 2022 wakati akizindua magari mawili ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, iliyokabidhiwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika maeneo mbalimbali nchini.

Pinda alisema Katiba hii ni kama Biblia au kitabu chochote cha dini, ambapo kila mmoja akisoma huja na tafsiri tofauti, jambo ambalo linaleta mkanganyiko kwa jami ambayo husikia na kuichambua vipengele vichache bila kuisoma.

Aliziomba taasisi zote zinazopata nafasi ya kuisemea Katiba kuwa zinapaswa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya uwelewa wa Katibab iliyopo kwa sababu ni mwongozo wa masuala mbalimbali katika utendaji haki za binadamu.

"Naziomba taasisi husika zinapopata nafasi zinapaswa kusaidia kutoa elimu kwa jamii juu ya Katiba iliyopo, hiyo itasaidia watu kuelewa suala la Katiba na sio kutembelea na vipengele viwili na kuvitafsiri tofauti," alisema Pinda.

Alisema kama Katiba ingekuwa mbovu basi serikali ingeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, na kuwa ndio maana imejikita kutoa elimu kwa jamii uwelewa kuhusu Katiba iliyopo na mpya ambayo inazungumziwa.

Alisema serikali inatambua umuhimu ndio maana imeamua kukutana na wadau wa vyama vya siasa kujadili nao.



Source : Nipashe
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages