Breaking

Wednesday, 23 March 2022

KAMISHNA MWAKILEMA AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA WA TANAPA

 



Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) William Mwakilema amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo hivi karibuni.


Tukio hiko lumefanyika leo Jumatano Machi 23, 2022 katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara.



Waliovalishwa vyeo ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Fidelis Kapalata na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Moses Nonga ambao kabla ya hapo walikuwa Maafisa Wakuu wa Uhifadhi.


Kamishna Mwakilema amewataka Makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele katika majukumu yake ya uhifadhi.


"Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye," amesema  Mwakilema.



Kamishna Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake ameahidi ushirikiano kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya shirika.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages