Ramon Abbas maarufu kama Hushpuppi amefunguliwa mashtaka mengine mapya ya utakatishaji fedha baada ya kufanya utapeli wa $400,000 sawa na Tsh million 926 akiwa gerezani Marekani.
Waendesha mashtaka wa Marekani waliwasilisha hati mbele ya Mahakama ya Wilaya ya California, Marekani siku ya jana Machi 16, pamoja na ushahidi kuhusiana na Hushpuppi kutenda uhalifu katika ofisi ya magereza.
Nyaraka za mahakama zilisema kuwa Hushpappi akiwa gerezani alishiriki katika ununuzi na ufujaji wa kadi za benki zilizopatikana kwa njia ya ulaghai kutoka kwa data iliyoibiwa za raia na wakazi wa Marekani.
Kati ya tarehe 28 Januari na 4 Machi 2022 maafisa wa usalama katika gereza hilo walibaini matumizi zaidi ya mtandao kwa Hushpappi wakijua kwamba alikamatwa kwa uhalifu unaohusiana na mtandao, walipata kibali cha kurekodi shughuli zake.
Mfumo maalum uliwekwa kwa ajili yake na shughuli zake zilirekodiwa kwa siku 7 na kubainika kuwa Hushpappi alikuwa akinunua kwa bidii kadi za benki za EIP kutoka soko la wahalifu wa mtandao ambapo aliporekodiwa alionekana akinunua kadi za benki 58 zenye thamani ya jumla ya $429,800 kwenye tovuti na kuziba pesa hizo.