Breaking

Thursday, 24 March 2022

PICHA: HATIMAE MZEE MREMA AFUNGA NDOA, MKE ASEMA ATAMRUDISHA UJANANI




Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Augustino Mrema leo Alhamisi Machi 24, 2022 amefunga ndoa na Doreen Kimbi katika kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

mke wa mzee mrema anayejulikana kwa jina la Doreen Kimbi amesema kuwa atamrudisha mzee mrema ujanani.

"Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi. Katika kipindi cha uchumba nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata. Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana" amesema Doreen

Ameongeza kuwa hajafata mali kwa mzee mrema

"Mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake"




TAZAMA PICHA HAPA CHINI









Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages